11 wafariki, shule zafungwa

0
661

Watu 11 wamefariki dunia na wengine 16 hawajulikani walipo huko Blantyre, Malawi
kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokana na kimbunga Freddy, kilichosababisha mvua kubwa.

Kufuatia athari hizo, Serikali ya Malawi imefikia uamuzi wa kufunga shule katika wilaya 10, kwa kuhofia kimbunga hicho ambacho pia kimesababisha uharibifu katika nchi jirani ya Msumbiji ikiwa ni pamoja na vifo vya watu 28.

Mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la Kusini mwa Malawi imeharibu miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya barabara na umeme.

Walimu na wanafunzi wamehimizwa kutumia mitandao na masomo ya redio wakiwa nyumbani, na shule zitapofunguliwa walimu wamehimizwa kutoa masomo ya ziada kwa muda uliopotea.