Bosso aachiliwa mateka

0
425

Kocha wa  timu ya mpira wa miguu ya Yong Sports Academy inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Cameroon, -Emmanuel Ndoumbe Bosso ambaye alitekwa nyara hapo jana, ameachiliwa huru.

Uongozi wa timu hiyo umethibitisha kuachiliwa huru kwa Bosso ambaye alitekwa nyara katika mji wa Bamenda wakati akielekea kwenye mazoezi ya timu hiyo na kuongeza kuwa kwa sasa amekabidhiwa kwa familia yake.

Msemaji wa timu hiyo ya Yong Sports Academy, – Wanchia Cynthia amesema hakuna malipo yoyote yaliyofanywa kwa watu waliomteka nyara kocha huyo ili aachiliwe huru  na haijafahamika  sababu za kufanya hivyo.

Wanchia  amesema kuwa huenda kauli zilizokuwa zikitolewa na mashabiki wa timu hiyo pamoja na matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Cameroon,  vimechangia kwa kiasi kikubwa kuachiliwa kwa Bosso.