Lema aliniambia nina kesi, nikamwambia rudi nazifuta

0
264

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hawachukulii wapinzani kama maadui, bali anawachukulia kuwa ni watu wanaomuonesha changamoto ili aweze kuzitatua.

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo alipokuwa akisalimiana na wananchi wa USA River jijini Arusha.

Amesema Mtanzania yeyote awe chama chochote cha siasa wanachotofautiana ni mawazo tu na fikra, lakini yeye hawachukulii wanasiasa wa upinzani kama maadui.

Amesema wanasiasa wa upinzani ni watu watakaomuonesha yeye pamoja na viongozi wengine kwenye serikali yake changamoto zilipo ili wazitatue na hivyo kukiimarisha zaidi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Kwa hiyo mdogo wangu Lema amerudi, ameniambia Mama nataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi’, nikamwambia nazifuta rudi, amerudi tuimarishe siasa si ndio?,” amesema Rais Samia na kuongeza kuwa
“Mwanaume ni yule anayejiamini, Mwanamke ni yule anayejiamini, kwa hiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini tupo vizuri na tutakwenda vizuri”.