Selena Gomez ampindua Kylie

0
260

Mwanamuziki na Mwigizaji Selena Gomez mwa nchini Marekani ameingia kwenye rekodi ya dunia ‘Guiness World Record’ kwa mara nyingine tena baada ya kumpindua mwanamitindo Kylie Jenner wa nchi hiyo na kuwa mwanamke mwenye wafuasi wengi zaidi katika mtandao wa Instagram.

Nyota huyo wa zamani wa Disney maarufu kwa wimbo wa Come & Get It, mwezi Februari mwaka huu alijinyakulia taji hilo kwa kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 381,580,525

Kylie aliyenyakuwa taji hilo mwezi Desemba mwaka 2021, yeye ana wafuasi zaidi ya milioni 290,683,268.

Selena (30), aliwahi kushika nafasi hiyo mwaka 2019 na kunyang’anywa taji hilo na Ariana Grande (29), kabla ya Kylie (25) kuwapita.