Rais Samia azungumza na viongozi aliowateua

0
175

“Kuna maswali mengi nimeyaona yakisemwasemwa kwenye mitandao, kwenye magazeti la kwanza huyu Mama ananyofoa watu wenye akili huku anawachukua huku, huku sasa nani atafanya?. Hao wote ni Watanzania na watafanyakazi popote na hakuna asiye na akili wote wana akili na kila mtu akiwa anaonekana ana akili zaidi na mimi namuhitaji zaidi.

Hivyo tutaendelea kunyofoa huko kuwaleta ndani waje watusaidie huku kwa sababu wakikaa nje kazi ni kuilaumu serikali bila kujua ugumu uliopo ndani ya serikali, wakiingia tutafanya nao watupe uzoefu wao waone yaliyopo serikalini kwa pamoja tuende.”

Rais Samia Suluhu Hassan