Messi afikisha magoli 700 ya klabu

0
195

Lionel Messi amefikisha magoli 700 katika ngazi ya klabu akiwa ni mchezaji wa pili katika ligi tano kubwa za Ulaya kufikisha idadi hiyo baada ya Cristiano Ronaldo.

Messi alifikisha idadi hiyo kufuatia goli lake moja katika ushindi wa magoli 3-0 ilioupata PSG dhidi ya Marseille.

Nahodha huyo wa Argentina alifunga magoli 778 katika michezo 672 akiwa na Barcelona, na tangu amejiunga na PSG tayari amefunga magoli 28.

Kutokana na mafanikio yake aliyoyapata katika Kombe la Dunia, Messi anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA ambayo itatolewa leo.

Kwa upande wake Ronaldo alivuka rekodi ya magoli 700 mapema msimu huu akiwa na Manchester United kabla ya kutimkia Saudi Arabia kujiunga na Al-Nassir akiwa na magoli 701.