Mgumba out Tanga

0
197

Rais Samia Suluhu Hassan amemhamisha Waziri Kindamba kutoka mkoa wa Songwe alikokuwa mkuu wa mkoa huo kwenda kuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga akichukua nafasi ya Omary Mgumba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Rais Samia pia amemteua Dkt. Francis Michael kuwa mkuu wa mkoa wa Songwe.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Michael alikuwa Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Christina Mndeme ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Sophia Mjema ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Itikadi
na Uenezi.