Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza Tanzania.
Dkt. Mpango amewakaribisha wawekezaji hao kuwekeza hasa katika miradi inayolenga kuleta mabadiliko chaya kwenye uchumi ikiwemo sekta ya kilimo, teknolojia ya mawasiliano, utalii, usafirishaji na nishati.
Makamu wa Rais ametoa ukaribisho huo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Kimataifa wa Biashara baina ya Tanzania na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, mkutano unaolenga kuvutia uwekezaji Tanzania.
Amesema serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini, ili kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Mkutano huo unaokutanisha wafanyabiashara takribani 600 kutoka Tanzania na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya unafanyika kwa muda wa siku mbili.