Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ni miongoni mwa abiria wa treni iliyokwama kwa takribabi saa mbili, huku sababu za treni hiyo kufanya hivyo hazijabainika.
Rais Ramaphosa alikua akitoka katika mji wa Mabopane uliopo kwenye jimbo la Guateng, kuelekea kwenye mji wa Bosman kuendelea na kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Mei Nane mwaka huu.
Rais Ramaphosa mwenyewe amesema kuwa kukwama kwa muda wa saa mbili kwa treni hiyo bila taarifa yoyote ni jambo lililozusha taharuki kubwa kwake na hata kwa abiria wenzake, kwani kwa karibu muda wa saa moja hakukua na ulinzi wowote katika eneo hilo.
Treni hiyo iliyotakiwa kusafiri kwa muda wa dakika 45, ilisimama ghafla na abiria hawakupatiwa taarifa yoyote.