Apona Ukimwi

0
339

Watafiti wametangaza kuwa mwanaume mmoja nchini Ujerumani aliyeishi na virusi vya Ukimwi tangu mwaka 2008, amepimwa na hakuna virusi vilivyoonekana kwenye vipimo hivyo.

Utafiti uliofanywa na watafiti 36 kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Ujerumani, Uholanzi, Hispania na Ufaransa na kuchapishwa kwenye jarida la Nature Medicine, umebaini kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 53 aliacha kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi mwaka 2018 baada ya kupandikizwa seli “stem cell transplant” mwezi Februari mwaka 2013.

Upandikizaji wa seli ni matibabu yanayohitaji umakini mkubwa na kwa kawaida huachwa kwa ajili ya wagonjwa wa saratani.

Watafiti hao wamesema mwanaume huyo ni watano kuthibitika duniani kupona kabisa ugonjwa wa Ukimwi.