Choo cha miaka 2,400

0
238

Mabaki ya choo cha zamani cha kuvuta maji (ku-flush) yamegundulika huko China katika jumba la malikale lililoporomoka katika jiji la kale la Yueyang, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Choo hicho chenye miaka kati ya 2,200 na 2,400, kina bakuli ambalo lilikuwa ndani ya nyumba na bomba lililoelekea kwenye shimo la nje.

Watumiaji wanadhaniwa kumwaga maji kwenye bakuli kila lilipotumiwa, ameeleza Liu Rui wa Chuo cha Sayansi ya Jamii cha China.

Inadhaniwa kuwa choo hicho kilichokutwa ndani ya Ikulu pengine kilitumiwa na Qin Xiaogong, aliyetawala kuanzia mwaka 381 hadi 338 kabla ya Kristo, Qin Xian’gong aliyetawala kuanzia mwaka 424 hadi 362 kabla ya Kristo au Liu Bang, mfalme wa kwanza wa Enzi ya Han mwaka 206 kabla ya Kristo hadi 220 baada ya Kristo.

Bakuli la choo, sehemu nyingine zilizovunjika, na bomba la kutolea uchafu nje viligunduliwa msimu uliopita wa joto.

“Kitu hicho cha kifahari huenda kilitumiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa Ikulu iliyopatikana katika jimbo la Shaanxi nchini China”. Mmoja wa wachimbaji Rui, aliliambia gazeti la China Daily.

“Ni choo cha kwanza na cha pekee kuwahi kugundulika nchini China. Kila mtu katika eneo hilo alishangaa na kisha sote tukaangue kicheko,” Rui aliliambia gazeti hilo