TMA : Hakuna madhara ya kimbunga Freddy

0
106

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema, inaendelea kufuatilia kwa kina mwenendo wa kimbunga Freddy na itatoa taarifa kuhusu kimbunga hicho pindi kutakapokuwa na haja ya kufanya hivyo.

Taarifa iliyotolewa na TMA kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, kwa wiki nzima imekuwa ikikifuatilia kimbunga hicho na kujiridhisha kuwa hakina madhara ya moja kwa moja kwa sasa katika maeneo ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, kimbunga Freddy kipo Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi karibu na Pwani ya Madagascar.

TMA imelazimika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kimbunga Freddy kufuatia habari za uwepo wa kimbunga Freddy zinazosambaa katika mitandao ya kijamii na kuzua taharuki kwa jamii.