Raja Casablanca yatupwa nje

0
658

Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, – Raja Casablanca ya Morocco wameondoshwa kwenye michuano hiyo pamoja na kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya AS Otoho d’Oyo ya Congo Brazzaville.

Raja Casablanca imeshinda mchezo huo wa ugeinini kwa bao Nne kwa Moja, lakini ushindi wa bao moja kwa bila wa ndugu zao timu ya Hassania Agadir ya Morocco dhidi ya Renaissance Berkane pia ya Morocco ulitosha kuwaweka kando mabingwa hao watetezi.

Timu zingine zilizofuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu Barani Afrika ni Gor Mahia ya Kenya , Etoile du Sahel ya Tunisia , miamba ya Misri – Zamalek, na CS Sfaxien ya Algeria.

Na kwenye kundi C, timu ya Al Hilal imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Nkana FC ya Zambia anayochezea Mtanzania Hassan Kessy kwa bao Nne kwa Moja.

Lakini pamoja na kufungwa, Nkana nayo imefanikiwa kufuzu kwa hatua hiyo ya Robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho.