Buti za laki 8

0
390

Buti za ‘Big Red Boot’ (BRB) zilizozusha gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na bei yake kuwa kubwa ikilinganishwa na muonekano wake zimeisha madukani siku tatu tu tangu zianze kuuzwa rasmi.

Buti hizo za chapa ya MSCHF (“Mischief”) chini ya Avant-garde zenye muonekano wa 3D ya katuni ya ‘Astro boy’ au mabuti anayovaa nyani wa Dora kwenye Dora the Explorer, yamefika hadi New York Fashion Week huku baadhi ya wasanii wakionekana kuyavaa sehemu mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwimbaji Ciara anaonekana kwenye pozi akiwa amevaa t-shirt kubwa na buti hizo zenye thamani ya dola 350 za kimarekani ambazo ni takribani shilingi 811,335 za kitanzania hadi dola 800 kwa maduka ya mitandaoni.