Ndoto ya Arsenal kutwaa ubingwa mashakani

0
224

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya England (EPL), Manchester City amepanda hadi kileleni mwa ligi baada ya kuifunga Arsenal 3-1, akijiimarisha kutetea taji hilo.

Arsenal sasa wamepoteza michezo mitatu kati ya minne ya mwisho kwenye mashindano yote, wakiwa nafasi ya pili, lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kwa kipigo hicho, City inaendeleza ubabe wake ambapo imeshinda michezo yote ya ligi iliyokutana na Arsenal tangu mwaka 2016, sawa na misimu saba sasa.

Ndoto ya Arsenal kutwaa ubingwa wa kwanza ndani ya miaka 20 inaanza kuingia doa, kufuata kufanya vibaya katika michezo ya mwisho na hivyo kupunguza ukubwa wa utofauti wa alama kati yake na Manchester City.