Wakazi wa kijiji cha Lingusanguse na wale wa kitongoji cha Semeni wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuwajengea daraja katika mto Ming’eng’e litakalounganisha maeneo yao.
Wakazi hao wamedai kuwa wakati wa masika wamekuwa wakishindwa kupata huduma muhimu kutokana na mto huo kujaa, hali inayosababisha pia shughuli mbalimbali za maendeleo kusimama