Makazi yaliyotumika Kombe la Dunia yepelekwa Uturuki

0
479

Qatar inapeleka nchini Uturuki nyumba zinazohamishika 10,000 ambazo zilitumika kama malazi wakati wa Kombe la Dunia la mwa 2022 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lliloikumba Uturuki na Syria.

Takribani watu 40,000 wanaaminika kufariki dunia katika matetemeko mawili ya ardhi yaliyozikumba nchi hizo mbili wiki moja iliyopita.

Zaidi ya watu milioni moja wameachwa bila makazi nchini Uturuki na idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi nchini Syria, mashirika ya misaada yametahadharisha.

Mfuko wa Maendeleo wa Qatar, chombo cha serikali kinachohusika na maendeleo ya kimataifa na misaada ya kigeni, ilituma video ya kundi la kwanza la malazi likitumwa katika maeneo yaliyoathirika.

Afisa mmoja wa Qatar alisema “Mipango ya Kombe la Dunia la 2022 kila mara ililenga malazi kama haya ya muda kutolewa.”