Hakuna mgogoro kati ya hifadhi ya Rwanyabara na wananchi wa Bushasha

0
142

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema hakuna mgogoro wowote kati ya wananchi wa kijiji cha Bushasha na hifadhi yoyote ya wanyamapori katika mkoa wa Kagera.

Ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Kagera, Conchesta Rwamlaza aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kumaliza mgogoro katika Mbuga ya Rwanyabara na kijiji cha Bushasha kata ya Kishanje wilayani Bukoba.

Amefafanua kuwa mgogoro uliopo wilayani Bukoba ni kati ya kijiji cha Kangabusharo katika vitongoji vya Nshisha, Kangabusharo na Kayaga na Hifadhi ya Msitu wa Ruasina ambao tayari umefanyiwa kazi na timu ya wataalamu.