Msanii Fulani afariki dunia

0
249

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mwanaharakati wa kutetea haki za wenye Ualbino Babu Sikare maarufu Albino Fulani amefariki dunia.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na mmoja kati ya marafiki zake wa karibu, msanii Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa za zaidi zinaeleza kuwa Albino Fulani amefariki dunia huko Columbus, Ohio nchini Marekani alikokuwa akiishi.