LeBron James aweka rekodi ya ufungaji bora NBA

0
206

LeBron James ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani ya NBA na kuipiku rekodi ya miaka 39 ya mkongwe Kareem Abdul-Jabbar.

Nyota huyo wa Los Angeles alifunga vikapu 38 kwenye
mchezo ambao timu yake hiyo ilipoteza kwa vikapu 133 kwa 130 dhidi ya Oklahoma City Thunder.

Nguli Kareem Abdul-Jabbar aliweka rekodi hiyo ya kuwa mfunga bora wa muda wote wa NBA mwaka 1984 ikiwa miezi nane kabla ya LeBron James hajazaliwa.

Mwenyewe LeBron James amesema ni jambo jema kwake kuingia kwenye rekodi za vigogo kama Kareem Abdul-Jabbar ambaye aliweka rekodi hiyo kabla ya yeye kuzaliwa.

LeBron James ni bingwa mara nne kwa taji la NBA na huu ni msimu wake wa 20 kuchezea ligi ya NBA ambapo kwa mara ya kwanza aliingia kwenye ligi hiyo na timu ya nyumbani kwao ya Claveland Cavaliers mwaka 2003 na mwaka 2010 akajiunga na Miami Heat ambako alitwa taji la NBA mara mbili akiwa na timu hiyo na akarejea tena Claveland Cavaliers ambayo aliisaidia kutwa taji la NBA mwaka 2016.

Mwaka 2018 akajiunga na Los Angeles Lakers ambayo alitwaa nayo taji lake la nne la NBA huku akiwa amecheza fainali 10 za NBA pia ametwaa medali ya dhahabu ya Olimpiki mara mbili na sasa amevunja rekodi ya Kareem Abdul-Jabbar ambae alicheza ligi ya NBA kwa misimu 20 kwenye timu za Milwaukee Bucks na Los Angeles Lakers ambapo kwa wakati wote alitwa taji la NBA mara sita.