Aua twiga na kuchoma nyama yake

0
254

Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wanamshikilia Michael Mwambaja kwa tuhuma za kuua Twiga mwenye uzito wa kilo zaidi ya 700 na kuchoma nyama yake usiku wa kuamkia hii leo.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Madundasi mkoani Mbeya, kijiji kinachopakana na Hifadhi hiyo ya Taifa ya Ruaha.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa askari hao wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wanaendelea kumsaka mtu mwingine anayedaiwa kushirikiana na Mwambaja katika tukio hilo.

Kukamatwa kwa mtu huyo kunafuatia msako uliofanywa na askari hao ambao pia wamemkuta na vitu mbalimbali.

Vitu hivyo ni pamoja na dawa za asili, ambazo mtuhumiwa huyo amedai ni za kumsaidia kutoonekana na askari pamoja wanyama na kuwafanya wanyama washindwe kukimbia.

Baada ya kuhojiwa, Mwambaja amesema aliua twiga na kisha kuchoma nyama yake kwa lengo la kuuza nyama yake.