Tutahakikisha namba za waliofariki hazitumiki vibaya

0
198

“Kama nilivyosema dhumuni la zoezi hili ni kupunguza wimbi la uhalifu linaloendelea, tunataka kuhakikisha kwamba namba zote zinazotumika zimehakikiwa kwamba mtu amethibitisha kwamba hii ni namba yangu. Lakini tunaishi kwa hiyo ina maana hata siku moja tu ikiongezeka kuna wanaofariki, kwa hiyo ni zoezi ambalo litakuwa na uendelevu ila tarehe 13 ni kwamba zote ambazo hazijahakikiwa zinaondoka kwenye usajili.

Lakini ina maana baada ya tarehe 13 kutakuwa bado kuna watu wanafariki hivyo kunaweza kuwa na laini ambazo zikatumika vibaya za watu ambao hawapo, hivyo kila baada ya muda inabidi tuwe tunahakikisha laini hizi ni za wahusika wenyewe.”

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari