Miili ya wanafamilia 16 kuagwa na kuzikwa Rombo

0
275

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nudrin Babu, leo anatarajiwa kuongoza mamia ya waombolezaji katika kuaga miili ya watu 16 waliofariki dunia tarehe 3 mwezi huu katika ajali ya gari wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Shughuli ya kuaga miili hiyo inafanyika katika viwanja vya hospitali ya Huruma wilayani Rombo na tayari
maandalizi yote muhimu yamekamilika

Baada ya kukamilika kwa ibada ya kuwaombea marehemu pamoja shughuli ya kuaga miili, leo yatafanyika
mazishi ya watu hao ambao ni wanafamilia.

Miili mitatu kati ya hiyo 16 inatarajiwa kuzikwa hapo kesho katika maeneo yaliyoandaliwa na familia zao.