Siku nne zimepita tangu tetemeko kubwa la ardhi lilipopiga eneo la Kusini mwa Uturuki na Mashariki mwa Syria na kusababisha vifo pamoja na uharibifu wa mali.
Mpaka sasa watu 12,873 wameripotiwa kufariki dunia katika tetemeko la ardhi nchini Uturuki na wengine 2,950 wakiripotiwa kufariki dunia katika tetemeko hilo hilo nchini Syria na hivyo kufanya idadi ya watu waliofariki dunia katika nchi hizo mbili kufikia 15, 823.
Nchi mbalimbali zimejitokeza kuzisaidia nchi hizo zilizokumbwa na tetemeko la ardhi ikiwemo Taiwan ambapo Rais wa Taifa hiyo Tsai Ing-wen pamoja na Makamu wake William Lai wametoa mshahara wa mwezi mmoja mmoja kila mmoja kwa ajili ya kuwasaidia watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki.
Zoezi la uokoaji bado linaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watu ambao bado wamenasa kwenye vifusi vya majengo mbalimbali yaliyoporomoka kutokana na tetemeko hilo.