Waliofariki kwenye ajali Tanga watambuliwa

0
189

Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga, Salma Sued ametaja majina ya baadhi ya wanafamilia waliofariki dunia katika ajali iliyotokea Korogwe mkoani Tanga na kusababisha vifo vya watu 17.

Wanafamilia hao waliofariki dunia ni pamoja na Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema, Godwin Mrema, Yusuph Saimon na Zawadi Mrema.

Wengine ni Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina Lamosa, Evelina na Cosmas Mrema.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Magira Gereza tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, barabara ya Segera – Buiko.

Imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu hao 17 huku 14 wakiwa ni wanafamilia na majeruhi 12.

Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni Mitsubishi Fuso na basi dogo aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar es Salaam kwenda Moshi, Kilimanjaro kwenye mazishi ambapo chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendokasi na uzembe wa dereva wa Fuso.