Dkt. Samia apokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Ruto

0
228

Rais Samia Suluhu Hassan, leo amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais William Ruto wa Kenya
uliowasilishwa na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo Moses Kuria.

Ujumbe huo uliowasilishwa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma,
umelenga zaidi kwenye kuongeza na kudumisha undugu na pia ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya Tanzania na Kenya.