Wadau wa sekta ya umma na binafsi wakutana

0
183

Serikali imepunguza mlolongo wa mfumo na taratibu za uwekezaji, ili kurahisisha shughuli za kibiashara na uwekezaji kufanyika katika mazingira mazuri.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji kwa maendeleo ya Tanzania.

Amesema sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo na uchumi wa Taifa, hivyo Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto, sera na sheria za kibiashara katika kuzalisha wawekezaji wengi kwenye sekta hiyo.

Dkt. Kijaji amebainisha kuwa licha ya uchumi wa dunia kutetereka, Tanzania imeendelea kuimarika kutokana na kutafuta mbinu za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.