Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewaomba wafanyabiashara nchini kupunguza bei za bidhaa hasa vyakula, ili kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi wa kipato cha chini.
Dkt. Mwinyi ametoa ombi hilo Ikulu, Zanzibar alipokutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara mbalimbali, ambapo wamejadili kupanda kwa bei za vyakula nchini.
Amesema bidhaa za vyakula ikiwa ni pamoja na mchele zimepanda maradufu, hali iliyozusha taharuki na kuzidisha ugumu wa maisha kwa wananchi.
Dkt. Mwinyi amesema haijawahi kutokea mchele kupanda bei kwa kiasi kikubwa kama ilivyo sasa na kuongeza kuwa mchele ni bidhaa yenye uhitaji mkubwa kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.
“Zanzibar mchele ndio kila kitu ni sawa na wenzetu Arabuni ukiadimika unga, kukosekana mkate kunakuwa na vurugu mitaani, hapa Zanzibar watu wetu tu Rahimu sana, lakini sasa hivi wamefikishwa pabaya sana, kilo elfu tatu mchele kubwa, haijahi kutokea, tujitahi Ramadhani inakuja na hili ni ombi langu kwenu.” amesisitiza Dkt. Mwinyi