Real Madrid na Barcelona nusu fainali Copa del Rey

0
363

Real Madrid na Barcelona zitakutana katika nusu fainali ya Copa del Rey. Mchezo wa kwanza utapigwa Santiago Bernabéu na mchezo wa marudiano utapigwa Camp Nou.

Droo ya mashindano hayo imefanyika leo mchana ambapo Osasuna itakutana na Athletic Club.

Mzunguko wa kwanza utachezwa kati ya Machi 1 au 2 mwaka huu huku michezo ya marudiano ikichezwa kati ya Aprili 4 na Aprili 6.