Ruksa mkulima kuuza mazao anavyotaka

0
200

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema hakuna mtu yeyote ana haki ya kuingilia uhuru wa kuuza au kununua mazao ya mkulima mara baada ya kuvuna.

Bashe amesema mkulima ana haki ya kuamua namna ya kuuza mazao yake popote kwa yeyote bila kuingiliwa mtu ama taasisi yeyote.

Waziri huyo wa Kilimo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa taarifa kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi za Uswisi na Senegal, ziara iliyojikita zaidi katika sekta ya Kilimo.

Ameongeza kuwa serikali inaendelea na juhudi za kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa na kuwataka wananchi kuwa watulivu.

Waziri Bashe amesema kwa sasa suluhu ya kudumu inatafutwa katika kukabiliana na changamoto hiyo.