Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera leo amewaapisha wakuu wa wilaya tatu za mkoa huo walioteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.
Walioapishwa ni Jaffar Haniu, mkuu wa wilaya ya Rungwe, mkuu wa wilaya ya Mbeya Benno Malisa na mkuu wa wilaya ya Kyela, Josephine Manase.
Akiwaapisha wakuu hao wapya wa wilaya, Homera amewataka viongozi hao kwenda kushirikiana na wanachi, kutatua kero zao pamoja na kusimamia mapato na matumizi ya halmashauri zilizomo ndani ya wilaya zao.
Wakizungumza mara baada ya kuapishwa, wakuu hao wapya wa wilaya wameahidi kufanya kazi kwa weledi na uaminifu.