Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ametangaza kuwa tatizo la kukatika kwa umeme lililokuwa linalikabili Taifa hilo limekwisha na maisha yanaendelea kama kawaida.
Nchi hiyo imejikuta katika mgogoro mkubwa wa kisiasa baada ya wanasiasa wawili nchini humo kuanza kugombea madaraka.
Maduro amesema kuwa Marekani na kiongozi wa upinzani nchini humo Juan Guido aliyejitangaza kuwa Rais wa serikali ya mpito, wameshindwa katika jaribio la kupindua serikali yake baada ya kukata umeme nchi nzima.
Huduma mbalimbali zilizokuwa zikitegemea umeme nchini Venezuela zililazimika kusimama kwa muda wa siku kadhaa ikiwemo huduma ya interneti kwa baadhi ya maeneo.
Nchi za Magharibi ikiwemo Marekani zimemtambua Guido kuwa Rais wa serikali ya mpito ya Venezuela na kumshinikiza Maduro kuachia madaraka, jambo ambalo kiongozi huyo analiita kuwa ni mapinduzi dhidi ya serikali yake.
Nchi za China na Russia pamoja na baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini zinamuunga mkono Maduro.
Nchi za China na Russia pamoja na baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini zinamuunga mkono Maduro.