Katika michezo mitano iliyopita ikizikutanisha Arsenal na Manchester City, Arsenal imepoteza michezo yote ambapo mara ya mwisho ilipata ushindi mwaka 2020.
Katika msimu wa mwaka 2022/23, timu hizo zitakutana mara tatu, ikiwa ni mara mbili kwenye Ligi Kuu ya EPL na mara moja kwenye Kombe la Shirikisho, mchezo ambao utapigwa leo usiku kuanzia saa 5 usiku.
Je! Arsenal itafuta uteja au City itaendeleza ubabe wao?
Tupe utabiri wako kuelekea mchezo huu ambapo pia unaaminika utatoa taswira ya mwenendo wa EPL.