Everton mbioni kumtangaza mrithi wa Lampard

0
247

Sean Dyche anatarajiwa kuwaa mikoba ya kuiona klabu ya Everton ambayo hivi karibuni imemfukuza kazi Frank Lampard kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Dyche na Marcelo Bielsa ambaye amewahi kuifundisha Leeds United ndio waliokuwa washindani wa kubwa kutwaa mikoba ya Lampard baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Everton.

Everton ambayo ni ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England itawakaribisha vinara wa ligi Arsenal katika Uwanja wa Goodison Park Februari 4 mwaka huu, wenyewe wakipambana wasishuke daraja, huku Arsenal wakitaka kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.