POLISI WAKUMBUSHWA KULINDA MIRADI YA TPDC

0
178

Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo Awadhi Juma Haji ametembelea na kukagua kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi mkoani Dar es Salaam na kituo cha makutano ya awali ya kupokea gesi asilia kilichopo Somangafungu, Kilwa mkoani Lindi.

Akiwa katika ziara hiyo amewaasa makamanda wa jeshi la polisi wanaosimamia maeneo hayo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia kanuni na misingi ya kiutendaji ya jeshi hilo.