Mwambe azikwa

0
240

Mazishi ya Pius Mwambe, mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) yamefanyika hii leo nyumbani kwake Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki pamoja watumishi wenzake wa TBC.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji Reuban Mlay amesema, Mwambe atakumbukwa kwa uchapakazi wake na ushirikiano mzuri na wenzake kazini.

“Mwambe alikuwa amestaafu lakini kutokana na umuhimu na weledi wake Shirika liliamua kumpa ajira ya mkataba ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa akitumikia Taifa.” amesema Mlay

Pius Mwambe alifariki dunia tarehe 22 mwezi huu katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.