Arsenal yaunyatia Ubingwa EPL

0
276

Arsenal imedhihirisha kuwa inautaka ubingwa wa Ligi Kuu ya England mwaka huu baada ya kuifunga Manchester United magoli 3-2 katika uwanja wa Emirates.

Ule msemo wa anayecheka mwisho hucheka zaidi umedhihirika katika mchezo huo ambapo Arsenal walitoka nyuma kwa goli moja, goli la mapema la Manchester, na kufanikiwa kuondoka na alama tatu.

Klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa London inalenga kumaliza ukame wa miaka 20 bila kutwaa taji hilo, ambapo mara ya mwisho walishinda msimu wa mwaka 2003/04.

Kwa ushindi huo Arsenal imefikisha alama 50, baada ya kushuka dimbani mara 19, ikiongoza ligi, ikifuatiwa na Manchester City yenye alama 45 baada ya kucheza michezo 20.