10 washikiliwa sakata la mbolea feki

0
189

Jeshi polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 10 kwa madai ya kuhusika na sakata la kuchakata na kuuza mbolea bandia kwa wakulima.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe, Hamis
Issah amesema hayo baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ikiendelea kupekua nyumba ya mfanyabiashara anayedaiwa kuwa muhusika mkuu wa mbolea hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuhakiklisha watuhumiwa wote wanaohusika na sakata hilo la
kuchakata na kuuza mbolea bandia kwa wakulima wanachukuliwa hatua.

Pia amewataka wakulima mkoani humo kuwa makini na mbolea wanazonunua na endapo wakibaini kuwa ni bandia watoe taarifa kwa maafisa kilimo wa kata zao.

Tayari Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA) imemfutia leseni mfanyabiashara anayedaiwa kuwa ndiye mmiliki wa mbolea hiyo bandia.