Mpanga ateuliwa na CAF

0
199

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limemteua Mwamuazi wa kati kutoka Tanzania Kassim Mpanga kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20).

Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika nchini Misri ambapo waamuzi wote walioteuliwa wanatarajiwa kufanya kozi ya maandalizi itakayofanyika kuanzia Februari 13 hadi 18 mwaka huu nchini Misri.