Kambi ya jeshi yashambuliwa

0
313

Wanamgambo wa Al Shabaab wa nchini Somalia wameshambulia kambi moja ya jeshi nchini humo.

Shambulio hilo limefanywa ikiwa ni siku moja tu baada ya serikali ya Somalia kudai kupata ushindi wa kihistoria dhidi ya wanamgambo hao baada ya kutwaa ngome muhimu ya wanamgambo hao.

Habari zaidi kutoka Somalia zinaeleza kuwa, gari lililokuwa limebeba milipuko liliegeshwa jirani na kambi hiyo ya jeshi dakika chache kabla ya watu wetu wenye silaha kuanza kushambulia na kulipua mabomu.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu idadi kamili ya vifo vilivyotokana na shambulio hilo katika kambi hiyo ya jeshi iliyopo kwenye mji wa Hawadley .

Akilihuhutubia Taifa kupitia redio ya serikali ya Somalia, Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Odowaa Yusuf Rage amesema askari watano wa ngazi ya juu wameuawa katika tukio hilo huku taarifa nyingine zikidai ni 11.