Shule zafunguliwa baada ya mlipuko wa kipindupindu

0
229

Wizara ya afya nchini Malawi imeruhusu kufunguliwa tena kwa shule za awali, msingi na sekondari baada ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Taarifa zilizotolewa na wizara hiyo zinaeleza kuwa, kwa sasa maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu yamepungua kwa kiwango kikubwa na kuruhusu kufunguliwa kwa shule na baadhi ya maeneo ya huduma za jamii yaliyofungwa kwa lengo la kuzuia maambukizi.

Hata hivyo wizara hiyo ya Afya ya Malawi imeeleza kuwa baadhi ya shule katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa kipindupindu zitaendelea kufungwa ili kufuatilia mwenendo wa maambukizi katika maeneo hayo.