Mwanafunzi ajiua baada ya kukataliwa na mpenzi wake

0
169

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Gunze Luhangija wa Kwimba Mwanza aliyekuwa akisomea Shahada ya Menejimenti ya Ushirika na Uhasibu (BCMA), amekutwa amejinyonga huku chanzo kikisemekana ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na kukataliwa na mpenzi wake aliuyekuwa anamgharamikia ikiwemo kumpangishia nyumba na kumnunulia simu aina ya iPhone 14.

Imedaiwa kuwa marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake siku chache baada ya kumnunulia simu janja hiyo hali illiyopelekea kuwa katika hali ya msongo wa mawazo.

Waliomfahamu marehemu wameeleza zaidi kuwa alishawahi kujaribu kujiua kwa kunywa sumu Januari 4 mwaka huu lakini aliokolewa.