Marhaba, mpira rasmi wa CHAN 2022

0
163

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) pamoja na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Umbro wamezindua mpira rasmi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yatakayoanza kutimua vumbi Ijumaa Januari 13, 2023 nchini Algeria.

Mpira huo umepewa jina la ‘Marhaba’ ikiwa na maana ya ‘Karibu.’

Michuano ya CHAN intarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 13, 2023 mpaka Februari 4, 2023 ambapo mchezo wa ufunguzi utawakutanisha wenyeji Algeria dhidi ya Libya