Nyota wa Simba, Peter Banda anaendelea na prograu maalumu itakayomrejesha kwenye ubora wake.
Mchezaji huyo hajaonekana uwanjani tangu mwishoni mwa mwaka 2022 baada ya kupata kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Ni kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars alipata maumivu alipoingia akitokea benchi na alifunga bao moja.
Ngoma ilikuwa nzito katika mchezo huo kwa kuwa waligawana pointi moja moja kwa kufungana bao 1-1.
Banda yupo Dubai na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Robertinho Oliviera, raia wa Brazil akishirikiana na Juma Mgunda ambaye ni mzawa.
Mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa Novemba 9, 2022 katika mchezo dhidi ya Singida Bog Stars.