Chongolo ampongeza Rais Samia

0
270

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo kwa niaba ya chama hicho amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Akitoa salamu za chama wakati wa matembezi maalumu ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Chongolo amesema “Chama cha Mapinduzi kimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, kwetu sisi Chama cha Mapinduzi hiyo ni fursa muhimu na kubwa sana kwani tunakwenda kuitumia kuelezea umma kazi ambazo serikali yetu inazifanya.”

Kwa upande mwingine, Chongolo ameahidi kuwa CCM itafanya shughuli hizo za kisiasa kwa kufuata sheria taratibu na miongozo ya serikali.