Vijana watakiwa kushiriki uchumi wa buluu

0
131

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kujiunga katika vikundi ili kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa buluu.

Rais Samia ametoa rai hiyo katika eneo la Paje, Kisiwani Unguja wakati akihitimisha maandamano ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) yaliyofanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesisitiza kuwa ni wakati wa vijana kujiunga katika vikundi ili kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa buluu na wao kunufaika na fursa zilizopo katika uchumi huo.

“Nataka kuwasihi vijana kujipanga na kujiunga katika vikundi ili kushiriki na kutumia fursa za uchumi wa buluu kujiletea maendeleo,” amesema Rais Samia.

Maandamano hayo yamehusisha pia viongozi wa juu wa CCM na jumuiya zake