Uwekaji Nembo Daraja la Tanzanite Wakamilika

0
190

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam umesema uwekaji wa nembo ya Tanzanite katika Daraja la Tanzanite umekamilika, hivyo kuwataka watumiaji wa daraja hilo kuendelea kulitumia huku kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kulinda miundombinu.

Aidha, TANROADS imewaomba radhi wananchi wote kwa usumbufu uliojitokeza wakati wa uwekaji wa nembo hiyo ambapo daraja lilifungwa tangu Januari 2, 2023.