TFF: Fei Toto bado ni mchezaji wa Yanga

0
253

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum bado ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba.

Uamuzi huo umetolewa baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko ikipinga hatua ya mchezaji huyo kuvunja mkataba bila kuwashirikisha.

Taarifa ya TFF imesema kuwa uamuzi kamili kuhusiana na shauri hilo utatolewa Jumatatu Januari 9,2023

Malalamiko hayo yalisikilizwa jana kwa kuhusisha pande zote mbili.