Waziri Ummy: Tunafuatilia video ya Tabora

0
340

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema timu ya wataalamu inafuatilia video ya watumishi wa afya iliyosambaa mtandaoni ikiwaonesha watumishi wa afya wakizozana huku mmoja kupinga kitendo cha vifaa tiba vilivyoisha muda wa matumizi kuendelea kutumika.

Katika taarifa yake kupitia mtandao wa Instagram Waziri Ummy amesema Timu ya Usimamizi Afya ya Mkoa (RHMT) wa Tabora na ya Halmashauri (CHMT) ya Wilaya ya Uyui wanafuatilia suala hilo na Serikali itatoa taarifa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa.


Aidha, amewatoa wananchi hofu akisisitiza kuwa “nchi yetu ina stock [akiba] ya vitendanishi vya kupima malaria (MRDT) ambavyo havija-expire [havijaisha muda wa matumizi] vya kutosheleza miezi 6.”