UWT: Tuko tayari kwa mikutano ya hadhara

0
144

Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, amesema wapo tayari kufanya mikutano ya kisiasa ya hadhara kwa kufuata taratibu zote, kujenga hoja zenye ushawishi na kuwaweka watu pamoja ili kujenga Taifa litakaloongea lugha moja.

Chatanda ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati akizungumza na wanahabari ikiwa ni siku moja tangu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atoe tamko la kuondoa zuio kwa vyama vya siasa vyenye usajili kufanya mikutano ya hadhara.

Amesema UWT kuanzia ngazi ya kata mpaka Taifa itaandaa mikutano ya hadhara yenye kutangaza siasa zilizopevuka, zisizo na matusi, kashfa, kubeza au kutweza utu wa mtu mwingine, na badala yake zitakuwa siasa za kuisemea ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020/25.